Jumamosi , 4th Dec , 2021

Kutoka Arusha, Motra The Future ameachia wimbo mpya “Weupe” ambao ni diss track kwa Kikosi Kazi ikiwa ni wiki 4 zimepita tangu P Mawenge wa Kikosi Kazi aachie wimbo wa “Nahamia Weusi”.

Kikosi kazi

Katika wimbo huu Motra anasikika akitaja wasanii wa Kikosi Kazi akianza na One Incredible, Songa na Azma Mponda.

“Kwanza Kikosi Kazi hakina kazi za kufanya. Hamjifunzi kwa Wakazi muziki sio tu kuchana”, mwishoni amemaliza na Azma.

“Joh hawezi kushuka eti kwa kupondwa na Azma mtu ambae ana force miaka 10 kutoka kwa lazima 
Crew yenu mnafanana style kama mchele wa basmart”.