Mchezaji wa muziki wa Bongo Mose Iyobo na Star wa Filamu Bongo Aunt Ezekiel
Akizungumza na eNewz Mose alisema kuwa kuna kitu ambacho watu hawafahamu ambacho ni kuwa, yeye anakaribia kuwa bwana harusi wa mzazi mwenzie huyo ''Mama Cookie''.
“Lakini ninavyoishinae ni ndoa tosha kwa sababu tunaishi kama baba na mama hivyo nataka kujithibitisha inabidi nifunge ndoa ili watu wani-verify kama instagram”,alisema Mose.
Pia Mose alisema kuwa hapendi watu wanavyomzungumzia vibaya mzazi mwenzie huyo wakidai kuwa eti ni mzee kwani angelikuwa hivyo yeye asingelisogea kwa kuwa angelikuwa kama anatembea na mama yake na kuongeza kuwa wakifurahishwa na uwepo wa mtoto wao Cookie kwa kuwa ndoa anaewafanya wao waendelee kuwepo pamoja.