Jumamosi , 19th Nov , 2016

Msanii Octopizzo kutoka Kenya ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na muziki wake wa rap kuwagusa wengi, amesema kitendo cha kuandamwa na maneno negative ya watu kwake ni sawa, kwani yeye ni mtu muhimu.

Rapper Octopizzo

Akizungumza kweny kipindi cha Friday Night Live cha East Africa Radio na East Africa Television, Octopizzo amesema yeye ni sawa na samaki mkubwa ambaye kila mtu anamuhitaji.

"Mimi ni sawa na big fish, when u are a big guy, every one wants a peace of you, unajua mti wenye matunda ndio unapigwa mawe, so i'm a big fish", alisema Octopizzo.

Octopizzo ambaye kwa sasa yuko nchini kwenye ziara yake kwa vyombo vya habari na kutangaza kazi zake zaidi, amezungumzia pia suala la yeye kufanya collabo na msanii mwengine wa rap nchini humo, Khaligraph Jones, na kusema ni suala ambalo linawezekana pale tu ambapo atalipwa.