Jumatatu , 11th Jan , 2016

Msanii mkongwe wa muziki Stara Thomas, amesema kuwa tatizo la mguu alilokuwa amepata katika mguu imezima ndoto yake ya kuingia katika siasa katika kipindi cha uchaguzi kilichopita.

Stara Thomas

Stara aliyekuwa na mpango wa kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum huko Mwanza ambapo ni nyumbani kwao, katika mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ameeleza kuwa, harakati za kisiasa zinahitaji mtu kuwa fiti ili kuweza kuhimili mikiki na mizunguko ya kujinadi, kitu ambacho hakikuwezekana kutokana na hali aliyokuwa nayo.

Nyota huyo amesema kuwa, mpango wake huo bado upo akiwa amelenga kujikita kwa nguvu zote mwaka 2020 wakati awamu ya uongozi uliopo sasa utakapomaliza muda wake madarakani.