Alhamisi , 12th Feb , 2015

Msanii wa muziki Mez B kutoka East Zoo Dodoma, amelazwa hospitali huko mjini Dodoma akiwa anasumbuliwa na maumivu ya kichwa na shingo, hali iliyomuweka chini ya uangalizi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

msanii wa bongofleva nchini Mez B

eNewz tumeongea na star huyu na kuweza kueleza kwa mashabiki hali yake ambayo imekuwa ikiyumba tokea mwisho wa mwaka na kuwaomba kumuwia radhi kwa kuchelewa kwa project zake mpya kutokana na hali inayomkabili.