Jumatano , 1st Jun , 2016

Msanii ambaye ni shabiki na anatamani sana kufanya kazi na Nyota wa Bongo Fleva Diamond Platinumz amejikanyaga baada ya kuulizwa anajiskiaje kuona lebo ya WCB inazidi kukusanya wasanii lakini yeye wanamsahau.

Msanii wa Bongo fleva Meda

Akizungumza na eNewz Meda alikosa jibu la yeye kutoingia katika lebo hiyo ya WCB mpaka leo hii pamoja na kuandika barua kwa mmiliki wa lebo Diamond kupitia katika nyimbo yake ya barua kwa Diamond na kudai kuwa kazi nzuri ndo zinakufanya watu wakutambue na ufike mbali na wala si kuwa sehemu fulani.

Japokuwa Meda alishapata nafasi ya kuonana na Bosi huyo wa WCB na kuweza kuzungumza naye maneno mawili matatu pamoja na kuonyesha hisia za wazi kupenda kufanya kazi na msanii huyo lakini mpaka leo bado Diamond amemfumbia macho huku akiendelea kusajili vichwa vipya katika lebo yake.