Mb Dogg alia na Serikali 

Jumatatu , 19th Jul , 2021

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Mb Dogg alia na Serikali juu ya watu wanaopiga pesa kupitia kazi zake kwenye platforms mbalimbali.

Picha ya Msanii MB Dogg

MB Dogg amefunguka kuwa kuna ukiukwaji wa Sheria za Hakimiliki hali inayosababisha wasanii wengi wakongwe kupitia wakati mgumu kwa kutonufaika na kazi zao, huku akiiomba Serikali kuingilia kati jambo hilo.

“Sheria za ukiukwaji wa HAKIMILIKI zipo na zifuatwe ili iwe fundisho kwa wadau na wasanii, pia kuwa makini na  majina yao kutumika vibaya”