Jumatatu , 14th Dec , 2015

Msanii Maurice Kirya ameibua gumzo nchini Uganda baada ya kunukuliwa akisema hana bahati na wanawake wa Uganda, jambo ambalo limepokelewa kwa hisia tofauti.

mwanamuziki nyota wa Uganda Maurice Kirya

Mwanamuziki huyo ambaye pia aliwahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa, sasa ameamua kuweka kambi yake Kenya kumtafuta mwanamke atakaye-uliwaza moyo wake.

Kirya ameapa kutorejea Uganda hadi atakapompata mwanamke wa kuishi naye anayemtafuta, baada ya kuzinguliwa na wanawake wa Uganda.

Hata hivyo baadhi ya wanawake wa Uganda wamesema kuwa Maurice Kirya kuachwa vibaya na Jemima, haina maana ya kuwa aache kutafuta mwanamke wa nchi hiyo kwani wapo wanawake waaminifu tu.