Jumanne , 28th Feb , 2017

Msanii kutoka kundi la 'Jambo Squad' Nigga C ameweka wazi leo katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio kuwa wimbo wake wa kipendacho roho kutofika mbali ni kutokana na familia ya mrembo aliyeonekana katika video hiyo kumtishia maisha.

Nigga C

 

Nigga C amesema kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo huyo ambaye alikuwa ni mwanafunzi wa kidato cha tatu na familia yake ilipogundua hilo ilianza kumfuatilia hali iliyosababisha atake kufanya maamuzi ya kuhama mji wa Arusha.

"Yule manzi alikuwa kanipenda sana, kipindi nafanya 'Kili Music Tour'  mtoto alitaka nizunguke naye akawa hataki kusikia habari za shule, kwa kuwa nilikuwa najali zaidi kazi nikamwambia mamilo wewe tulia kwanza maana huu ni muda wa kazi, ndiyo maana hata ilipokuwa ikishika chati za juu sikuwa na kimbelembele nayo" - Nigga C

Hata hivyo Nigga C amesema anaishukuru familia hiyo kwa maamuzi ya busara waliyoamua kuyachukua baada ya kuangalia maisha yake na umri wake wakagundua ni mtoto.