Jumatano , 22nd Apr , 2015

Malaika, staa wa muziki ambaye amerejea na nguvu na mtindo mpya kupitia rekodi yake inayokwenda kwa jina 'Sare', amesema ngoma hiyo kumewashangaza wengi wakipata changamoto kuelewa kama ni yeye ndiye aliyefanya ngoma hiyo.

Msanii wa miondoko ya bongofleva Malaika

Malaika amesema, rekodi hiyo imepata mapokezi mazuri na mipango yake ni kufanya video yake hapahapa nchini, akimtarajia director wa kazi hiyo ambaye ni mwanadada kutoka UK kutua hivi karibuni kufanya kazi hiyo.