Jumatano , 10th Jun , 2015

Msanii maarufu wa muziki nchini Uganda mwenye makazi yake nchini Finland Mad Ice hivi sasa ameelekeza nguvu zake katika kufanya matayarisho ya video ya wimbo wake mpya alioubatiza jina 'End of The World'.

Msanii wa muziki wa nchini Uganda Mad Ice

Hii ni moja ya kazi yake mpya ambayo imefanyiwa utayarishaji na producer Tarmo Makipaya wa nchini Finland.

Mkali huyo ambaye hivi sasa yupo nchini Finland ameongea na eNewz kuhusiana na kufanya kazi na producer huyo nyota kutoka mjini Helsinki nchini Finland.