Jumamosi , 8th Nov , 2014

Rapa wa muziki wa kizazi kipya, Mabeste ambaye wiki hii ameachia video ya Nishauri baada ya kungojewa kwa muda na mashabiki wake, amesema kuwa, kazi hii mbali na ubora wake, ni mfano mzuri kwa wasanii wengine kuwa inawezekana kufanya kazi nzurI

Mabeste

Mabeste amesema kuwa, kazi hii imetumia akili ya mipango ama planning, kitu ambacho kimeifanya kuwa rahisi na katika ubora unaotakiwa, vilevile ikiwa pia ni kwaajili ya kuonesha wasanii wengine kuwa hapa nchini kuna maeneo ya kutosha tu ya kufanya kazi nzuri kama yale ambayo wanayafuata nnje ya nchi.