Msanii wa filamu na muziki nchini Tanzania Zuhura Abdul Kadri aka Lolo Da Princess
Zuhura anayetamba na wimbo wake 'Wanitesa' ameongea na eNewz na kusema kuwa changamoto ambazo zinamkabili kwanza ni kujijengea idadi kubwa ya mashabiki wake ili kuweza kujitangaza zaidi katika tasnia hiyo.
Aidha, mwanadada huyo ametoa historia fupi kuhusiana na kuingia katika fani hiyo baada ya kujulikana ndani ya filamu yake ya kwanza iliyobatizwa jina 'Before My Death'.