Jumapili , 7th Feb , 2016

Mwanamuzi wa RNB kutoka nchini Tanzania Steve Rnb ameachia video ya wimbo wake wa Listen akiwa nchini Ujerumani na kusema wimbo huo ni maalum kwa ajili ya siku ya Wapendanao.

Mwanamuzi wa RNB kutoka nchini Tanzania Steve Rnb

Steve Rnb ambae yupo nchini Ujerumani kikazi kwa mkataba maalumu amesema kwa kuwa siku ya wapendanao hatakuwepo nchini Tanzania lakini kwa video hiyo ya wimbo wa Listen itawawakilisha vema Wapendanao.

Steve amesema wimbo huo ambao amefanya na Mtayarisha wa video Mtanzania amefanya katika nchi mbili tofauti ambazo ni Tanzania na Kenya, katika kupata mazingira tofauti zaidi.