Jumanne , 13th Feb , 2018

Wengi wanamfahamu kwa umahiri wake aliouonyesha kwenye filamu ya sarafina akiwa na umri wa miaka 15 tu, filamu ambayo ilitikisa karibu Afrika nzima na baadhi ya nchi za ugahibuni.

Lakini jina lake halisi ni Leleti Khumalo, muigizaji na sasa ni mtangazaji wa radio, pia ni mwana harakati wa haki za binadamu.

Katika maisha yake baada ya kuwa maarufu alipitia changamoto nyingi kama kuolewa na mwanaume ambaye alikuwa akimtesa.

Mwaka 2016 star huyo aliamua kuweka wazi juu ya ugonjwa unaomsumbua, ambao unaathiri kiasi kikubwa cha ngozi yake,unaojulikana kama 'Vitiligo'.

Moja ya chombo cha habari cha Afrika Kusini kilimnukuu akisema kuwa “imechukua muonekano wangu lakini niko sawa, sitaki maisha yangu yawe kuhusiana na hali niliyonayo, kwani bado mimi ni yule yule muigizaji, mama na mke”.

Akisimulia zaidi kuhusu hali hiyo, leleti amesema alijigundua akiwa na miaka 24, mwanzoni alikuwa na hofu huenda mume wake angeacha kumpenda lakini baadaye alijikubali, na kuamua kufurahia maisha yake.

UFAHAMU UGONJWA WA VITILIGO

Vitiligo ni ugonjwa ambao unaathiri ngozi, unaotokana na kuharibiwa kwa cells za kutengeneza rangi ya ngozi zinazojulikana kama (melanocytes). Chanzo halisi cha celi hizi kushambuliwa bado hakijajulikana kitaalam, hivyo kupata ugumu wa kujua tiba sahihi ya ugonjwa huu.

Celi hizi zikishaharibiwa ngozi huanza kubadilika rangi kwa kuweka vidoa vyeupe, na mara nyingi huonekana zaidi kwa watu wenye ngozi nyeusi, ingawa ugonjwa huu unaathiri watu wote na wa rika zote.

Kitaalam Vitiligo hauambukizi isipokuwa unaweza kurithi kutoka kwa wazazi kutokana na genes anazobeba binadamu kutoka kwa wazazi, lakini pia baadhi ya celi za mwili zikijishambulia zenyewe, hauna madhara kwa kuhatarisha maisha (kuua) zaidi ya kubadili rangi yako ya ngozi.

Watu wenye ugonjwa huu mara nyingi hutumia lotion za sun screen ili kuzuia ngozi isipate madhara yatokanayo kwa kupigwa na jua kali, hasa kwa nchi zenye jua kali.

Kwa wagonjwa wa vitiligo wanashauriwa kumuona daktari mara tu anapoona dalili zake, ili kumpa dawa za kurestore rangi ya ngozi ambayo imeanza kupotea, lakini haizuii kutosambaa kwa ugonjwa.

Nikikufahamisha zaidi, msanii marufu duniani ambaye kwa sasa ameshafariki, Michael Jackson alikuwa ni muathirika wa ugonjwa huu na inasemekena ndio sababu ya kuamua kubadilisha rani ya ngozi yake, naye muigizaji mkongwe wa Bollywood, Amitabh Bachchan ameshawahi kusumbuliwa na ugonjwa huo.

Tazama picha za watu walioathiriwa na ugonjwa huo