Chidi Beenz
Kamanda Nzowa amesema kuwa tukio la kukamatwa kwa msanii huyu mkubwa, ni nafasi ya jamii na vijana kujifunza na kuachana na dawa hizi ambazo madhara yake kwa jamii ni makubwa.
Chidi baada ya upekuzi alipatikana na kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi, tukio ambalo limeendelea kuzua maoni tofauti kutoka kwa watu mtandaoni wakati huu ambapo anasubiri hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.