Mona Gangstar ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa nafasi hizo wasanii wa Bongo wanazihitaji sana ili kukuza muziki wao.
“Wasanii wenzetu wa Afrika wanakubali kufanya kolabo na sisi kwa sababu wao wanajitangaza zaidi, hiyo ni dalili moja wapo ya muziki kukua, kwa sababu ukishirikiana na mtu maarufu watu lazima watataka kusikiliza kwa nini ameshirikiana na huyu”, alisema Mona Gangstar.
Hivi karibuni wasanii wengi wa Tanzania wamekuwa wakivuka mipaka na kuwashirikisha wasanii wakubwa wa nje ya Tanzania, na kufanikiwa kuutangaza muziki wa Bongo fleva kwenye nchi nyingine hata nje ya Afrika.