
Camera ya eNewz ya EATV ilimtafuta na kutaka kujua kulikoni..! ambapo alifunguka na kusema kuwa collabo hiyo bado ipo palepale na kwamba inasubiri wakati wake ukifika, itakuwa hewani.
Alisema kwa kawaida katika kamati yake huwa wanakaa na kuangalia ni ngoma gani itoke na kwa wakati gani ambapo kamati hiyo ndiyo iliyoamua ngoma ya Waya itoke sasa badala ya ile aliyofanya na Davido.
“Waya nahisi ni wimbo ambao nimeamua kuutoa sasa na siyo huo tu nina ngoma nyingi sana nzuri ambazo ziko ndani kwahiyo kikubwa tunachoangalia ni timing tu, kwa hiyo sasa hivi nimeona nitoe waya kwanza na siyo kama collabo na Davido haipo, ipo na imeshakamilika lakini muda ukifika nitaitoa na siyo Davido tu, nina ngoma pia na YCEE na Falz na nyingine nyingi kali sana, mimi na team yangu tunakaa na kuangalia kwa sasa ni ngoma gani itoke na sasa tuliona Waya utatikisa ndiyo maana tumeutoa”
Pia Joh Makinni aliongeza kwa kusema kuwa kila muziki aliorekodi ni mkubwa kwa hiyo mashabiki bado waendelee kukaa tayari na kuendelea kusapoti muziki wake