Jumamosi , 1st Mar , 2014

Msanii wa muziki Koffi Olomide leo hii atatumbuiza huko nchini Zimbabwe katika sherehe ya harusi ya binti wa rais wa nchi hiyo, Bona Mugabe anayefunga ndoa na mchumba wake wa siku nyingi, Simba Chikore ambaye anafanya shughuli za urubani wa ndege.

Msanii huyu tayari ameshatua huko Zimbabwe tokea siku ya Jumatano akiwa na rais Robert Mugabe ambaye walitoka naye pamoja huko Congo ambapo ndipo alipopatiwa mualiko huu wa heshima wa kutoa burudani katika harusi.

Harusi hii inatarajiwa kuzua gumzo la aina yake hasa kutokana na mpunga ambao rais huyu ametajwa kuutoa kwaajili ya kuhakikisha kila kitu kinakwenda katika mstari, huku wageni wazito zaidi ya 4000 wakiwa wamealikwa katika sherehe hii.