Alhamisi , 15th Mei , 2014

Rapa Keko kutoka nchini Uganda, amebadilisha muonekano wake kwa kunyoa nywele zake zote kichwani na kubakia na kipara.

Rapa Keko

Mtindo huo umezua hisia na maoni tofauti kutoka kwa umati mkubwa wa mashabiki wa msanii huyu mahiri.

Kufuatia mtindo huu wa nywele, Keko ambaye amezoeleka kwa kutokelezea na muonekano wa kigumu unaokinzana na jinsia yake, amegawanya mashabiki wake katika sehemu mbili, upande mmoja ukimsapoti kuwa amependeza kutokana na mtindo huu, wakati upande wa pili wakiona kuwa amekosea na muonekano huu umekuwa ni wa kigumu sana kwake.

Keko ambaye anachukua maneno haya yote kama maoni ya mashabiki wake, kwa sasa amerudi tena kwa kishindo katika chati mbalimbali, kupitia ngoma yake inayokwenda kwa jina Fly Solo ambayo ameitoa hivi karibuni chini ya usimamizi wa Sony Music.