Jumanne , 31st Mei , 2016

Msanii mkongwe wa muziki wa rumba nchini Mzee King Kikii, Mzee wa kitambaa cheupe ametangaza kolabo na wasanii wa Bongo fleva atakaeweza kufanyanaye kazi .

Msanii mkongwe wa muziki wa rumba nchini Mzee King Kikii

Akizungumza na eNewz King Kikii alisema kuwa ni vyema sana kwa wasanii vijana wakashirikiana na wazee ili kuwajuza vilivyovingi kuhusu mziki ambavyo wao hawavijui hasa katika suala zima la digito.

“Muziki wa siku hizi unavitu vingi sana ambayo sisi wazee wengi wa zamani hatuvijui kwa hiyo ni vizuri hawa wasanii vijana wasiogope waje tu tufanye kazi pamoja,” alisema King Kikii.

Pia King Kikii alimtaja Diamond na A.Y ni moja kati ya wasanii anaotamani sana kufanya nao kazi muda wowote tu watakapokuwa tayari kufanya kazi pamoja naye.