
Kanye West Na Mama Mtoto Wake Kim Kardashian katika Muonekano wa Kurasa ya Mbele ya Vogue
Kim Kardashian mwenye umri wa miaka 33 ametokea akiwa amevaa gauni lililoacha wazi mabega yake huku akiwa mikononi mwa Mkali wa Hip Hop Mchumba wake na baba wa mtoto wake Kanye West.
Kichwa cha habari cha gazeti hilo kimewapamba "Kim na Kanye kwa kuwaelezea kuwa ni wapenzi wanaoongoza kwa masuala ya kwenda sawa na fasheni, na kuongeza kuwa pia ni wachumba ambao wanazungumziwa zaidi duniani.
Katika picha nyingine wawili hao wanaonekana wakitembea Jangwani na wakipata wakati mzuri kwenye ndege binafsi. Mtoto wao North West wa miezi 9 pia ametokelezea katika gazeti hilo.
