Khadija Kopa
Akipiga story kupitia eNewz ya EATV Khadija Kopa amesema kwa sasa anahitaji kupata wadhamini ili kuweza kufanya video nzuri kwani yeye anajua kuimba lakini hajui maswala ya uongozi hivyo anatamani kupata usimamizi ili kuweza kutengeneza kazi nzuri zaidi.
Pia amemalizia kwa kusema kwa sasa anajipanga ili arudi na muziki wa kisasa na kuwasihi mameneja wanaotamani kufanya kazi na yeye wajitokeze wasiogope umaarufu wake.