Jumamosi , 22nd Mar , 2014

Msanii Kenzo wa nchini Kenya ameweka wazi kuwa baada ya kipindi cha changamoto kubwa kwa fani yake ya muziki, ambapo alipoteza mkataba na lebo ya Ogopa, kwa sasa anaona mwanga katika muziki wake akiwa msanii huru anayeweza kufanya kazi mahali popote.

Taarifa pia zinaweka wazi kuwa jambo lililompa nguvu zaidi Kenzo ni hatua ya Ogopa kuamua kumuachia kazi zake zote ambazo alikuwa amezifanya chini yao, kazi ambazo zilikuwa bado hazijatoka.

Itakumbukwa kuwa hapo awali msanii huyu alitangaza kwa masikitiko makubwa kupoteza matumaini na muziki wake, baada ya lebo ya Ogopa kusitisha mikataba yake yote na wasanii wake, bila kueleza sababu hasa ya kuchukua uamuzi huo.

Tags: