Kalipina amjibu Wema kuhusu kupigwa

Jumapili , 12th Sep , 2021

Msanii wa HipHop Kalapina Nabii Koko amemjibu Wema Sepetu kwa kusema kwamba mwanamke hapigwi bali kuna njia za kumfanyia kama ukiona mwanamke wako ana maneno sana.

Picha ya Wema Sepetu na Kalapina

Kalapina amejibu hilo baada ya ujumbe wa Wema Sepetu kusema mtu kupigwa na 'baby' wake kuna raha yake na yeye binafsi ana-enjoy kupigwa.

"Mwanamke hapigwi, ukiona mtu anampiga mwanamke huyo ni 'bushaman' kwa sababu wao ndio wana mambo hayo, mwanamke anapigwa kwa zawadi ukiona kelele nyingi we mpe zawadi tu" amesema Kalapina

Kalapina ameongeza kusema kwenye upande wa mahusiano yeye ni mwamba na anamjua Wema Sepetu labda amemaanisha kupigwa kwa aina nyingine.