Jumatatu , 21st Apr , 2014

Msanii wa muziki, Kaligraph kutoka nchini Kenya, ameweka wazi kuwa, mafanikio aliyoanza kuyavuna sasa kutoka katika muziki, ikiwepo kazi zake kununuliwa sana mtandaoni, ni kazi ya miaka mingi sana na alianza kwa kulipwa pesa ndogo sana akitumbuiza.

Kaligraph

Rapa huyu ambaye muziki wake umeanza kueleweka kwa kasi sasa, amesema kuwa kutokana na hali kuwa ngumu alikuwa anafanya kazi ya uchekeshaji ambayo ilikuwa ngumu sana kukubalika na watu katika kipindi cha mwanzoni.

Kaligraph amesema kuwa, anajivunia kutoka alipotoka na ameweka wazi kuwa kukulia kwake huko Kayole Kenya kumekuwa na mchango mkubwa katika muziki wake na ujumbe anaojaribu kufikisha kwa wapenzi wa muziki wake.

Tags: