Alhamisi , 7th Mei , 2020

Kumekuwa na stori ambazo zinaeleza kwamba mkali wa RnB Bongo Jux, aliwahi kuwa na mahusiano na msanii wa filamu Jacqueline Wolper kipindi cha nyuma, japo watu wengi walikuwa hawafahamu.

Msanii wa RnB Juma Jux na staa wa filamu Jaqcueline Wolper

Sasa kuhusiana na hiyo ishu Jux ameeleza kipindi yupo kwenye mahusiano na staa huyo wa filamu, hawakuachana vizuri ndiyo maana hakuna ukaribu kati yao au hata kusapotiana kwenye kazi zao.

Akipiga stori na eNewz ya East Africa TV Jux amesema  "Kipindi cha nyuma nilikuwa naye, inategemea mahusiano yanapoishiaga kutokana na mazoea, kwa upande wangu haikuwa sawa sana, lakini nilielewa kutokana na maisha baadaye kila kitu kikawa sawa, sasa hivi tuko poa yeye ana maisha yake na mimi nina maisha yangu, hatuna tatizo lolote ni vya muda sana hivi".

"Kwani ni lazima anisapoti au awekewe lawama zote hizo, mimi sikasiriki kabisa na siangaliagi hivyo vitu, wafuasi ambao mimi ninao kwenye Instagram yangu, alionao Ben Pol au Wolper ni walewale tu, usikasirike kwa sababu mtu hajapost kazi yako" ameongeza.

Video kamili tazama hapa chini