Jumatano , 16th Apr , 2014

Mwigizaji maarufu wa filamu nchini Tanzania, Blandina Changuka maarufu kama Johari kwa jina la kisanii, leo hii ameshiriki katika kipengele cha Kikaangoni Live cha ukurasa wetu facebook, ambapo wapenda burudani wameweza kumuuliza maswali mbalimbali.

Johari ametumia muda wa saa mbili kujibu moja kwa moja maswali kibao ambayo mashabiki wake kutoka pande mbalimbali za Tanzania wamemkaanga nayo, na kuyajibu kwa ufasaha katika muda huo wote.

Katika mahojiano yake na eNewz, Johari amewataka mashabiki wake kufahamu kuwa, Japokuwa hajaonekana katika filamu sikunyingi, Yupo katika game na kampuni yake ile ile ya RJ, akishirikiana na Vicent Kigosi ama Ray, huku akiwataka wapenzi hawa wa kazi zake kupuuzia taarifa zote za uvumi kuhusiana na yeye kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Ray, Ostaz Juma vilevile.

Kumsikia Johari akizunguza kwa undani juu ya mambo haya endelea kutazama eNewz kila siku, na endelea kuwa sehemu ya familia kubwa ya wapenzi wa ukurasa wa facebook wa EATV, shiriki ukurasa huu na marafiki na Like pia kama bado hujafanya hivyo na kumbuka, Wiki ijayo tunakuletea staa mwingine mkali ambaye utachat naye moja kwa moja.

Inaweza kufuatilia maswali na majibu ya Johari kwa mashabiki wake hapa; https://www.facebook.com/eatv.tv/photos/a.159892260691867.39844.15730328...