
Wasanii wa HipHop ambao ni ndugu Joh Makini kulia, kushoto ni Nikki wa Pili
Joh Makini amesema hayo kwenye kipindi cha SalamaNa ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Alhamisi kuanzia 3:00 usiku ambapo alikuwa anawataja wasanii wa HipHop ambao anawakubali.
"Kwenye kizazi changu mimi kuna marapa wakali wengi tu kama Lord Eyes, Gnako na FidQ lakini Nikki wa Pili simuweki hapa, yeye ana 'era' yake pia" amesema Joh Makini
"Mimi na Lord Eyes tumetoka mbali tangu mihangaiko ya Arusha hadi kuja Dar na kukaa pamoja, hali yake ambayo aliipitia wote ilituhuzunisha lakini na hatukuwa na chakufanya ulikuwa wakati mgumu kwetu" ameongeza
Joh Makini, Lord Eyes, Nikki wa Pili na G Nako ni wasanii wa HipHop ambao kwa pamoja wanatokea kwenye kampuni ya Weusi.