Alhamisi , 18th Jun , 2015

Staa wa muziki wa injili nchini Kenya, Jimmy Gait ametangaza mpango wa kurejesha fadhila kwa mashabiki wake wapenzi kwa kutoa zawadi ya pikipiki kwa wale watakaofanikiwa kushinda katika shindano la kucheza alilolianzisha.

Jimmy Gait

Staa huyo ameeleza kuwa, ataendesha mpango huo kwa wiki 5 ambapo wapenzi wa kazi zake watatakiwa kumtumia video inayowaonesha wakicheza ngoma yake mpya ya Dathima, na yule atakayefanya vizuri zaidi atajipatia pikipiki mpya.

Jimmy amechukua hatua hii kutoa msukumo kwa wapenzi wengi zaidi wa muziki kusikiliza kazi yake hiyo mpya, na pia kuwafikishia ujumbe wa maombi na matumaini, hususani kwa wale wanaopitia wakati mgumu.