
JB amesema hayo leo mchana kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio, kwamba kuifanya akili ya binadamu kusahau kitu alichokiacha msanii aliyekuwa juu sio kazi rahisi.
Msanii huyo ametoa mfano wa aliyekuwa mkali wa Filamu za mapigano na Karate duniani Bluce Lee, ambaye alifariki wakati yupo katika kiwango cha hali ya juu, leo ukimueleza mtu kwamba Jackie Chan anafanya vizuri zaidi yake atakataa.
''Kanumba alifanya vizuri kwa muda mchache sana kisha Mungu akamchukua, wakati anafanya vizuri ndio hapo hapo mshumaa ukazima, sio rahisi kumuaminisha mtu kwa kiwango alichofanya Kanumba na alipoishia kuweza kufananisha na sasa kwakuwa alifanya vizuri zaidi ila bado waliopo wanafanya vizuri,'' amesema.
JB ameongeza kuwa Kanumba alikifikisha Kiwanda cha Filamu pazuri kwa kiwango chake, ila kila 'Industry' kuna wakati inapanda wakati mwingine inashuka na anaamini sasa wunarudi vizuri.