Jumatano , 4th Feb , 2015

Msanii Jaguar, ameibuka na kuamua kuvunja ukimya kwa mtindo wa aina yake kufuatia kitendo cha msanii Iyanya wa nchini Nigeria, kumsema kuwa ni mzembe ambapo ameweka picha mtandaoni akiwa katika hali ya kicheko cha kejeli kutokana na kauli hiyo.

Msanii Jaguar wa nchini Kenya

Sambamba na picha hiyo, Jaguar ameambatanisha na maneno "when @iyanya says iam lazy…..", kuonesha kuwa huu ni muendelezo wa uhasimu kati yao huku mitaa ikisubiri kuona kama star huyo wa Nigeria atajibu lolote kutokana na kitendo hicho.

Ugomvi wa mastaa hawa umetokana na kauli ya Jaguar kuwa wanigeria hawapendi muziki wa Afrika Mashariki ufanikiwe, akitolea mfano wa msanii huyo kukataa kusambaza video ya kolabo waliyofanya pamoja - One Centimetre Remix, licha ya kumtumia na kumuomba kufanya hivyo.