Jumanne , 15th Oct , 2024

Muigizaji na mchekeshaji Idris Sultan amehoji suala la mwanaume kumvisha/kuvisha pete mchumba wake kwa kupiga magoti limeanzia wapi sababu jambo hilo hajalisoma katika dini.

Picha ya Idris Sultan

"Hivi mwanaume anapopiga goti kumvisha pete mwanamke akimuomba kuwa mke wake imeanzia wapi na lini? Kwenye dini sijaisoma".

Mshindi huyo wa Big Brother Africa mwaka 2014 Idris amehoji hilo kupitia mitandao yake ya kijamii kama Instagram na X.