Ijumaa , 21st Aug , 2015

Msanii wa miondoko ya Soul na RnB nchini Tanzania Hisia ameonyesha furaha yake kwa kumpongeza mama yake Anna Mghwira ambaye ameteuliwa kugombea urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT - Wazalendo,

Msanii wa miondoko ya Soul na RnB nchini Tanzania Hisia

Hisia amesema kuwa hii ni njia moja wapo kubwa kwake kutokana na kwamba ni mwanaharakati na kujihusisa kwake katika masuala ya jamii.

Mkali huyo pia amegusia kuwa Mama yake ni mzaliwa wa mkoa wa Singida akiwa ni mwanasheria na mwanaharakati katika kuwasiadia akina mama na watoto, hivyo ni wazi hatua yake hii ya kugombea urais ni yenye mafanikio makubwa kwake na nchi nzima.