
Happiness Watimanywa - Miss Tanzania 2013-14
eNewz imelifuatilia zoezi hili kwa ukaribu mkubwa na kushuhudia namna ambavyo Happiness anavyojibu kwa umakini maswali mbalimbali aliyoulizwa na mashabiki wake na wadau wanaomfuatilia masula ya ulimbwende.
Baada ya kutoka Kikaangoni, eNewz ilikutana na Happiness kuzungumza naye na mrembo huyu akasema kuwa amevutiwa kwa namna ambavyo zoezi zima limeenda leo, swali kubwa kwake likiwa ni namna ambavyo amepata mafanikio na taji la Miss Tanzania katika umri mdogo ambapo amesema kuwa hakuna siri zaidi ya kujiamini katika kila lengo unalojiwekea.
Baada ya Happiness, sasa kaa tayari kuchat na staa mwingine mkali juma lijalo tena katika Kikaangoni Live, ambayo inakujia kupitia ukurasa wetu www.facebook.com/eatv.tv pekee.