Jumatatu , 3rd Jan , 2022

Ni ujumbe wa Omary Nyembo 'Ommy Dimpoz' baada ya kuanza mwaka mpya 2022 ambaye anasema tusikate tamaa kwani hakuna aliyesomea maisha cha msingi ni kupambana, kuwa na nidhamu na juhudi ili kufikia ndoto zetu.

Picha ya msanii Ommy Dimpoz

Ujumbe huo ameandika kwenye page yake ya Instagram unaeleza kuwa "Cha muhimu ni kupambania ndoto zetu na kuwa focused hakuna aliyesomea maisha, ukiwa na nidhamu na juhudi huku ukimuomba Mungu basi jua wakati wako utafika na riziki yako itaongezeka wala tusioneane choyo pale mwenzako anapopiga hatua".

"Tusikate tamaa wala kuhuzunika pale unapopata vikwazo kwenye utafutaji wetu kwani hata mitume ilipigwa vita na kuchukiwa itakuwa wewe mtoto wa Binti Saidi".