Jumanne , 15th Jul , 2014

Muigizaji nyota wa filamu nchini Tanzania Irene Uwoya tayari ameachia kidokezo cha filamu yake mpya aliyoibatiza jina 'Kisoda' ambayo imesheheni nyota wakali nchini akiwemo nguli wa filamu Mzee Majuto.

muigizaji wa bongo movies nchini Irene Uwoya

Irene ambaye ndiye muongozaji wa filamu hiyo mpya ya kusisimua ameongea na eNewz kuwa yupo nchini Afrika Kusini akiweka mambo yake sawa kwa ajili kuizindua rasmi filamu hiyo ambayo shooting yake imefanyiwa nchini Uturuki.

Aidha filamu hiyo ya 'Kisoda' ambayo inahusu maswala ya dansi ndani yake imeongozwa na kupigwa picha na John Kallage ambapo amewasihi pia mashabiki wake kuwa baadae atamtaja msanii mkubwa aliyeshiriki ndani ya muvi hiyo.