Alhamisi , 13th Nov , 2014

Mke wa msanii Amini Mwinyimkuu, Farida Bashir ambaye pia na yeye ni msanii wa muziki amesema kuwa, maisha yake ya kisanaa kwa sasa akiwa kama mke staa huyo yapo katika nafasi nzuri zaidi akiwa anatarajia kufanya mambo makubwa hivi karibuni.

msanii wa muziki Farida akiwa na mumewe ambaye pia ni msanii Amini

Farida ama Namcy V kwa jina la Kisanii, akiwa na ujauzito ambao hakuwa tayari kuweka wazi ni wa muda gani, ameiambia eNewz kuwa yeye pamoja na Amini kwa sasa sanaa zao zimekuwa kitu kimoja, na hapa anafafanua zaidi juu ya hili.