Jumanne , 15th Nov , 2016

EATV imeendelea kutoa elimu juu ya kupiga kura kwa msanii unayempenda awe mshindi wa EATV AWARDS, kwenye kipengele alichopendekezwa.

 

Zoezi hilo ambalo limeanza Ijumaa ya tarehe 11 Novemba 2016 na linatarajiwa kufungwa siku mbili kabla ya utoaji wa tuzo, limekuwa na hamasa kubwa kwa mashabiki, baada ya kuonekana wakiulizia kwa undani jinsi ya kupiga hizo.

Akitoa maelekezo ya jinsi ya kupiga kura Brenda Killeo ambaye ni mmoja wa waratibu wa tuzo hizo, amesema unaweza ukapiga kura kwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwa kuandika code ya msanii kwenye kipengele husika, na kuituma kwenda namba 15777.

Kwa watu walio nje ya Tanzania unatuma code number ya msanii kwenda namba +25574615777, au unaweza ukatembelea tovuti ambayo ni www.eatv.tv/awards, na utaruhusiwa kupiga kura mara moja tu kwa siku (saa 24) kabla hujapiga tena endapo utapenda.

Ujumbe mfupi utagharimu shilingi 150 za kitanzania, lakini ukipiga kura kwa kupitia kwenye tovuti ya www.eatv.tv/awards ni bure kabisa.

Tags: