Jumanne , 30th Oct , 2018

Baada ya kusambaa kwa tetesi na picha ikimuonyesha msanii wa muziki wa Injili Emmanuel Mbasha  na muigizaji wa filamu Tanzania Jackline Wolper wakiwa wanakunywa kinywaji kilichohisiwa ni pombe, Mbasha ameibuka na kukanusha tetesi hizo na kudai kuwa alikuwa anakunywa soda.

Jackline Wolper kushoto akiwa na Emanuel Mbasha.

Akiongea na eNEWZ, Mbasha amesema watu wamemjia juu kwa kukaa karibu na Wolper na kusema akiendelea kukaa karibu na  Wolper atampoteza na pengine anaweza akafanya mambo ambayo hayaendani na wokovu wake kama watu walivyomzoea kwamba yeye ni mtu wa dini.

"Mimi na Wolper ni marafiki wa karibu na ukweli ni kwamba mimi nampenda Wolper kama dada yangu na namkubali kwa kazi zake anazozifanya hata hivyo naamini kwamba na yeye ananipenda kwa kuwa tumekuwa karibu kwa muda mrefu sasa"aliongea Mbasha.

Mbasha alimalizia huku akitolea maelezo picha ambazo zimesambaa mitandano zikimuonyesha akiwa karibu na Wolper na kusema kwamba picha hizo zilitokana na kazi ambayo waliipata kwa pamoja ikawakutanisha na kuwaweka karibu.