Alhamisi , 20th Oct , 2016

Ikiwa amsha amsha za EATV AWARDS zikiendelea kwenye kila kona ya viunga vya nchi za Afrika Mashariki, wadau wa sanaa wametoa maoni mbalimbali kuhusu tuzo hizo kubwa Afrika Masahriki.

Egna Msuya Mdau wa sanaa.

Wakizungumza kwenye kipindi maalum cha EATV AWARDS kinachorushwa na East Africa Television, wadau hao wamesema tuzo hizo ni kubwa na zina lengo la kuinua sanaa ya Afrika Mashariki, hivyo wasanii wachangamkie fursa, kwani kwao ni soko la ajira na pia zitaleta hamasa kubwa kwenye kazi zao za sanaa.

Pia wadau hao wamesema wana imani kuwa EATV AWARDS hazitaishia hapa iwapo wasanii wenyewe watazipa kipaumbele, hivyo ni muhimu kwa wao kuzithamini ili zifike ngazi ya kimataifa ambapo itaruhusu hata wasanii wa nje ya Afrika waweze kushiriki.

EATV AWARDS zitafikia kilele chake tar 10 Desemba 2016, ambapo zitatolewa tuzo 9 kwa wasanii wa filamu na muziki wa Afrika Mashariki, pamoja na tuzo moja ya heshima.

Tags: