Jumanne , 24th Nov , 2015

Staa wa muziki Dully Sykes ameeleza namna ambavyo katika kipindi cha nyuma msanii kabla ya kuingia studio, analazimika kujipanga, akiwa na rekodi ya kukutana na watayarishaji muziki wakali wasiotaka mchezo hata kidogo kutoka kwa wasanii wazembe.

Staa wa muziki Dully Sykes

Dully ambaye amemtolea mfano Bonnie Luv, amesema kuwa, katika mazingira hayo ilimlazimu msanii kujipanga sana kuepuka hata kupigwa makofi, hii pia ikiwa ni moja ya sababu ya kuwafanya wasanii wa zamani kuwa bora zaidi ya wale wanaoibuka sasa.