Ijumaa , 1st Jul , 2022

Legend wa mziki wa Bongofleva Dully Sykes amesema wimbo wake hunifahamu ina historia ya ukweli kwa sababu kuna mwanamke alikuwa analazimisha kuwa naye kwenye mahusiano walipokutana Manyoni Singida.

Picha ya Dully Sykes

"Historia ya hunifahamu ni ya ukweli, ilianzia Manyoni Singida ikaja Dar yule msichana sasa ni marehemu alikuwa anaitwa Zamzam, kuna jambo lilitokea huko siwezi kulizungumzia kuhusiana na upoteaji wa simu ambao nilienda na wenzangu".

"Baada ya hapo yule msichana alirudi akaniambia haitaki tena ile simu wala hana mpango nayo, akasema anahitaji kuwa na mimi, sasa kwa kipindi kile nilikuwa na mwanamke naishi naye, nikamwambia asije kwangu ataniharibia mapenzi yangu". amesema Dully Sykes 

Chanzo PlanetBongo ya East Africa Radio kila siku ya J3 mpaka Ijumaa kuanzia saa 7:00 mchana mpaka 10:00 jioni.