Jumatano , 29th Jul , 2015

Staa wa muziki Dully Sykes, katika safari yake kama mtayarishaji muziki kando na kuimba, amemtaja P Funk Majani kama prodyuza ambaye amekuwa msaada mkubwa kwake kwa kumfundisha mambo mengi juu ya kutengeneza muziki.

staa wa miondoko ya bongofleva nchini Dully Sykes

Dully katika orodha yake hiyo pia amemtaja Marco Chali na Pancho Latino kutokana na moyo wao wa kumuinua katika safari hiyo, akiwa sasa mmiliki wa studio yake mwenyewe na ngoma kadhaa zikiwa tayari zinafanya vizuri katika mzunguko.