Dudu Baya
Akipiga story ndani ya eNEWZ, Dudu Baya alikuwa na haya ya kusema “kwa hiyo ndo maana Director kama Adam juma analalamika wasanii wanakimbilia nje ni kweli kwa kuwa wenzetu nchi za nje wanaenda na muda na kutafuta location za nyimbo pia”.
Dudu Baya alizidi kufunguka kuhusu utendaji kazi mbovu wa studio za hapa nchini, ambapo amesema, “Hata hivyo ukienda studio za Bongo unakaa siku nzima kuanzia asubuhi mpaka jioni kwa kuwa hawajajipanga vizuri wakati kwa nchi za wenzetu huwezi kukutana na msanii mwenzio studio sana sana mtakutana getini tu”.




