Jumatatu , 23rd Jun , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Dr. Hilderman katika jitihada za kujaribu kupooza mioyo ya waumini na viongozi wa dini ya kikatoliki waliokerwa na kitendo chake cha kuvaa joho la maaskofu jukwaani.

Dr. Hilderman akitumbuiza jukwaani

Dr. Hilderman amerekodi ujumbe wa kuomba msamaha na kuusambaza katika vyombo mbalimbali vya habari ambapo katika rekodi hii, Dr. Hilderman amekiri kulitambua kosa lake, na kutaka kusamahewa na kuyapatia nafasi mambo mengine kuendelea, huku akisisitiza kuwa hakuwa na lengo la kumuudhi yeyote akisema kuwa alichokifanya kilikuwa ni kwa ajili yake na si kwa ajili ya kanisa.

Baada ya kuanza kusambazwa kwa ujumbe huu wa maombi ya msamaha, jamii inaendelea kusubiri kwa hamu kusikia ni nini majibu kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo huko Uganda ambao mpaka sasa hawajajibu chochote.