Jumatano , 29th Jun , 2016

Kama ilivyo kawaida yetu huwa tunazipata zilizo chini na kuzileta juu baada ya kuibua stori kuwa Dogo Janja aka Janjaro akienda kwao Arusha anafikia gesti kwa kuwa wazazi wake wanaishi kwenye nyumba ya kupanga.

DOGO JANJA

Dogo Janja amesema ni kweli huwa anashukia gesti kwa ajili ya kuweza kulinda jina lake na kulinda hadhi yake ili kuzuia watu wasimuone one kwa kuwa huwa mara nyingi akienda huko anafanya shoo.

Hata hivyo Dogo Janja amesema ni kweli wazazi wake wanaishi nyumba ya kupanga lakini yupo mbioni kumalizia mjengo kwa ajili ya wazazi wake na yeye ndio anajua ni jinsi gani anaitunza familia yake.

Janjaro anasema yeye ndiye wa kwanza kuimba na kusema Mayoung wanapenga na wameamua kujitaja lakini wakati anaimba watu walimuona mchokozi na anatafuta kiki.