Jumamosi , 22nd Sep , 2018

Mashabiki wa msanii wa muziki nchini Dogo Janja, wameoneshwa kukerwa na kauli ya msanii huyo aliyoitoa katika mtandao wa twitter, ambayo wengi wao wameashiria kama anataka kujiua.

Msaani Dogo Janja

Hayo yote yamekuja baada ya msanii Dogo Janja kuweka ujumbe ndani ya mtandao huo akisema “Sina Urafiki na Dunia Yenu!” Kauli iliyopata komenti za wadau wengi wakisema.

www.eatv.tv imemtafuta Dogo Janja kuelezea hayo ambapo amesema, kauli hiyo inatoka katika wimbo wake mpya anaotarajia kuachia hivi karibuni,unaoenda kwa jina la “ “IMANI” huku akikataa kuzungumzia mahusiano yake na Irene Uwoya na kusema kauli hiyo haihusiani na maisha ya ndoa yake kwa sasa.

Tumekuwa tukishuhudia kuwepo kwa matukio yanayopelekea watu wengi kujiua hususani watu maarufu duniani kutokana na “stress” hofu za maisha au mahusiano. Wasanii Avicii na Mac miller ,waliripotiwa kupoteza maisha kutokana na stress walizokuwa nazo ndani ya mahusiano yao.

Dogo Janja amedaiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na mpenzi wake Irene Uwoya, hali inayoashiria kuvunjika kwa ndoa ya wawili hao.