msanii wa miondoko ya bongofleva Ommy Dimpoz
Aidha msanii huyo amegusia kuwa inaonekana uzito unawekwa zaidi kwa upande wa video siku hizi, kuliko upande wa utayarishaji wa ngoma yenyewe, ambao ndio msingi wa kazi.
Kwa mujibu wa Ommy Dimpoz, Gharama za Video huonekana ni kubwa zaidi kutokana na vitu ambavyo msanii huhitaji kuongezea katika video, juu ya ile gharama ya Director ya kuongozea Video.
Staa huyo amesema kuwa, licha ya mfumo wa kiserikali kukaa vibaya bado, kuna nafasi ya ma-producer pia kuweka gharama zao za kufanyia kazi katika kile kiwango wanachoona itawalipa, kikubwa kikiwa ni kufanya kazi nzuri na kujiamini.