Jumatatu , 9th Jun , 2014

Msanii Diamond Platimunz ametoa ya moyoni kuhusiana na kilichotokea baada ya safari yenye ushindani mkubwa ya kuwania tuzo kubwa kabisa za muziki Afrika kumalizika mwishoni mwa wiki bila kupata tuzo hata moja.

Diamond na Davido

Moja kwa moja kutoka Durban Afrika Kusini, Diamond Planumz baada ya kukosa tuzo katika kinyanganyiro hiki kikubwa, amekiri kuwa suala la kushindwa lipo katika kila mashindano, kwani uwepo wake katika tuzo hizo umempa nafasi kubwa ya kujenga ukaribu na wasanii wa kimataifa.

Diamond ambaye mbali na kukosa tuzo alifanya bonge la show, vile vile ameweka wazi kuhusiana na project kubwa za kimataifa ambapo hivi sasa mkali huyo anatarajia kufanya kazi na msanii Iyanya wa nchini Nigeria hiyvo mashabiki wake wakae mkao wa kula kusubiria kazi nyingi kutoka kwake.